JINA LAKO LINAANZIA NA HERUFI GANI?FAHAMU MAANA YAKE APA .YAPO FROM A-Z!
TATHMINI YA MAJINA KUTOKANA NA HERUFI ZA MWANZO ZA MAJINA HAYO
HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa,
anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye
tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda
Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.
HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na
hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anap
otaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika,
mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa
wabunifu na wanaopenda mawasiliano.
HERUFI D
Mwenye jina
linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu
wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye
mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu.
Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho
nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye
huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.
HERUFI G
Mwenye
jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na
nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya
watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali
ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina
linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara,
hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo
mengi, mchoyo na mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia
na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati
mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli,
mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa.
Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo
thabiti,mashuhuri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za
watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika
na hali ya kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na
herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri
kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana,
mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na
mwepesi kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na
mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye
uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
HERUFI P
Mwenye jina
linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima
kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye
mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q
ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana
uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza
sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu
mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote
anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na
herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye
maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa
kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada
ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa
ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye
tamaa na aliyekosa maamuzi.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.
HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita
kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye
tamaa na hufanya mambo ya hatari.
HERUFI X
Mwenye jina
linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye
anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.
HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na
hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na
husababishia kupoteza bahati katika maisha.
HERUFI Z
Mwenye
jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani.
Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni